Search This Blog

Tuesday, September 14, 2021

Upinzani wataka jeshi kufanikisha uchaguzi haraka

 


Kiongozi wa muda mrefu wa upinzani nchini Guinea, Cellou Dalein Diallo ameutaka uongozi wa kijeshi nchini humo kuunda serikali ya mpito na kutangaza muda wa kufanyika uchaguzi baada ya mapinduzi ya juma lililopita.


Diallo amesisitiza kuwa jeshi kwa sasa lazima lithibitishe nia yake ya kurejesha mamlaka kwa raia kama walivyoahidi wakati mapinduzi dhidi ya rais Alpha Conde Septemba 5.Diallo anamshutumu rais Conde aliyeondolewa madarakani kwa kujiangamiza mwenyewe baada ya kuwa na fikra ya muhula wa tatu madarakani kwa kusema ukomo wa madaraka kikatiba hauna nafasi kwake.


Akizungumza katika mahojiano yake na shirika la habari la AP, Diallo amesema Conde amekisaliti kiapo chake na kuliingiza taifa katika mgogoro mkubwa na kumwelezea mpinzani wake huyo wa muda mrefu kama dikteta.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...