Search This Blog

Sunday, September 12, 2021

Mkuu wa IAEA yuko Iran kwa mazungumzo juu ya mzozo wa nyuklia


Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kudhibiti matumizi ya nishati ya nyuklia IAEA Rafael Grossi yuko nchini Iran leo Jumapili kwa mazungumzo juu ya mvutano kuhusu mradi wa nyuklia wa taifa hilo, siku chache baada ya shirika hilo kuikosoa Tehran kwa kutoonyesha ushirikiano. 


Grossi, aliyewasili Tehran jana jioni anatarajiwa kukutana na Makamu wa Rais wa Iran Mohammad Eslamu ambaye pia anaongoza shirika la nishati ya Atomiki la nchi hiyo. Ziara ya Grossi inajiri wakati mazungumzo ya mjini Vienna yamekwama juu ya kuunusuru mkataba wa nyuklia wa mwaka 2015 unayoijumuisha Iran na mataifa yenye nguvu duniani. 


Katika mazungumzo hayo, Iran inatakiwa kupunguza uzalishaji wake wa madini ya Urani. Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump aliiondoa Marekani kwenye mkataba huo mwaka 2018 na kurejesha vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Iran.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...