Wapiganaji wa Taliban wamelichukua jumba la kifahari la mjini Kabul la mmoja wa maadui wao wakubwa-mbabe wa kivita na Makamu wa Rais wa zamani Abdul Rashid Dostum.
Jumba hilo la kifahari, limeonyesha kwa kiasi gani watawala wa zamani wa Afghanistan walivyokuwa wakiishi maisha ya anasa. Taliban imesema mali za watawala hao wa zamani zilitokana na ufisadi wa miaka mingi serikalini.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP ilipofanya ziara katika jumba hilo la kifahari, ni kuwa lina muundo wa kipekee na viti vya starehe wakati Waafghani wengi wa kawaida wanaishi kwenye lindi la umaskini. Abdul Rashid Dostum mwenye umri wa miaka 67, ameitoroka nchi hiyo na kwenda Uzbekistan.

No comments:
Post a Comment