Search This Blog

Wednesday, September 29, 2021

Korea kaskazini yarusha kombora la pili kwa chini ya saa 24

Korea Kaskazini imedai kuwa ilifanikiwa kujaribu kombora llake jipya linaloitwa Hwasong-8, siku ya Jumanne.

Vyombo vya habari vya serikali vilisema kombora hilo jipya lilikuwa moja wapo ya mifumo "mitano muhimu zaidi" ya silaha iliyowekwa katika mpango wake wa maendeleo ya kijeshi wa miaka mitano.

Walilsema kombora hilo jipya ni "silaha ya kimkakati", ambayo kwa kawaida inamaanisha uwezo wa nyuklia.

Uzinduzi wa Jumanne ni dalili nyingine ya teknolojia ya silaha iliyo nayo Pyongyang, licha ya kukabiliwa na vikwazo vikali.

Uendelezaji wa mfumo huu wa silaha ... [umeongeza] uwezo wa taifa wa kujilinda kwa kila njia," kituo cha habari cha serikali ya Korea Kaskazini KCNA kilisema.

Uzinduzi wa hivi karibuni pia uliashiria jaribio la tatu la kombora nchini humo mwezi huu.

Makombora ya Hypersonic yana kasi zaidi na wepesi zaidi kuliko yale ya kawaida, na kuifanya iwe ngumu sana kwa mifumo ya ulinzi wa makombora kuyazuia, kulingana na shirika la habari la AFP.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...