Search This Blog

Wednesday, September 29, 2021

Waziri Ummy azindua Baraza la wafanyakazi TARURA

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Ummy Mwalimu mapema leo amezindua Baraza la Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA).

Akizundua Baraza hilo amewapongeza  Mwenyekiti aliyechaguliwa Ndugu Joseph Sasi na Makamu mwenyekiti Azimina Mbilinyi pamoja na wajumbe wote 102 watakaoongoza Baraza hilo kwa kipindi cha Miaka mitatu.

“ Ninyi ni wawakilishi wa Wafanyazi takribani 1264 wa TARURA hivyo ninyi ndio mmebeba maono, matamanio na mawazo ya wote hao hivyo mtumie baraza hili kwa majadiliano ya pamoja ya msingi na kiutendaji yatakayoleta tija kwa watumishi wote wa TARURA.

“ Baraza hili litumike kujadili malengo na mawazo ya taasisi pamoja na maslahi ya watumishi, na mtu yeyote akiona kuna tatizo apeleke kwenye Baraza la Wafanyakazi nmaana ndio sehemu sahihi ya kutatua changamoto za wafanyakazi tulitumie baraza ipasavyo ili kuleta ushirikiano na mshikano kati ya wafanyakazi na TARURA.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...