Search This Blog

Wednesday, September 8, 2021

Bitcoin yapingwa siku ya kwanza baada ya kuhalalishwa El Salvador

 


Waandamanaji wenye hasira nchini El Salvador, wanapinga kuhalalishwa kwa teknolojia ya fedha ya kidigitali.

Gharama ya Bitcoin siku ya Jumanne, ilishuka katika kiwango cha chini zaidi katika mwezi, ilishuka kutoka $52,000 (£37,730) mpaka $43,000 .

Mwanasiasa mmoja wa upinzani alisema kushuka kwa fedha hiyo ya kidigitali imesababisha taifa hilo kupoteza kiasi cha dola milioni tatu ($3m).

Uzinduzi wa Bitcoin nchini El Salvador umekuwa tofauti na kile ambacho Rais Nayib Bukele alikuwa anafikiria wakati anaanza jaribio lake la kishujaa.

Makampuni kama ya Apple na Huawei hawakuiunga mkono serikali katika mpango wake uliofahamika kama 'Chivo', na watumiaji walikuwa wanajitoa baada ya kuona kuwa hawawezi kuendelea na usajili katika makampuni hayo.

Lakini mfumo huo wa Chivo ilianza kupokelewa na majukwaa zaidi na ulikuwa unakubaliwa na kampuni kama Starbucks na McDonald's.

Serikali ilikuwa imetoa $30 ya Bitcoin kwa kila raia ili kuwahamasisha kukubali mfumo huo.

Ilidaiwa kuwa bitcoin ingeweza kukomboa $400m kwa mwaka katika malipo ya kutuma fedha nje ya nchi.

Hata hivyo kwa kutumia takwimu za benki ya dunia na serikali , BBC ilipiga hesabu na kupata kukaribia $170m.

Ed Hernandez anauza duka la familia huko San Salvador ambapo wateja wanaweza kununua mchele maharage na bidhaa za usafi.

"Wakati huu wa janga la corona ni sawa kutumia fedha ya digitali ," aliiambia BBC, anasema inamsaidia kupata hela halali na sio feki.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...