Zikiwa zimetimia siku 74 tangu ilipojulikana kutoweka kwa askari Emmanuel Govela, Jeshi la Polisi mkoani hapa limesema uchunguzi wake umekuwa mgumu na wanamchukulia ni mtoro kazini.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Onesmo Lyanga alisema jana kuwa kazi ya kumtafuta Govela (39) ambaye taarifa za kutoweka kwake zilijulikana Juni 26, 2021 imekuwa ngumu kwa upande wao kutokana na mazingira ya tukio lenyewe.
Lyanga alisema wanamchukulia Govela ni mtoro kazini kwa sababu aliondoka bila utaratibu.
Aliwaomba wote wanaofahamu na kumuona askari huyo watoe taarifa ili waone jinsi ya kushirikiana nao kuhoji.
“Sisi tunaendelea kumtafuta na kama mna vyanzo vyovyote vya kujua yuko wapi, basi itakuwa ni jambo jema ili na sisi tumhoji.”

No comments:
Post a Comment