Search This Blog

Wednesday, September 8, 2021

Mamia wakimbia makazi yao Laikipia, Kenya



Mamia ya watu wamekimbia makazi yao wakati ghasia zilipotokea katika hifadhi ya Laikipia iliyopo bonde la Ufa nchini Kenya.

Mamlaka wametoa wasiwasi wao juu ya watu wenye silaha ambao walikuwa wanapambana na polisi.

Zaidi ya watu 12 wameuawa, wakiwemo wiki iliyopita walikufa sita.

Milio ya risasi ilisikika majira ya mchana, moshi ukionekana huku nyumba na shule zikiwa zinaungua.

Wakazi wakiwa wanakimbia makazi yao ambayo wamekaa kwa miongo.

Washambuliaji katika hifadhi binafsi ya Laikipia pia wanalisha mifugo yao kwa jeuri kwenye mashamba ya mahindi la wakulima wasio na ulinzi.

Eneo lililoathirika, wakazi wanadhani kuna mtu anataka waondoke.

Kamishna wa eneo la Bonde la Ufa,George Natembeya amedai wavamizi hao wana bunduki aina ya M16 , ambazo haziuzwi nchini humo.

Polisi wa Kenya huwa wanatumia G3 na AK47, ambapo mara nyingine watu wasiokuwa na vibali hutumia kufanya ujambazi.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...