Search This Blog

Tuesday, August 24, 2021

Zuma aomba kuchangiwa gharama za kukabiliana na kesi



Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma anauomba umma kumchangia fedha zitakazomuwezesha kukabiliana na kesi inayomkabili ya tuhuma dhidi ya rushwa.

Katika kurasa rasmi ya twitter ya taasisi yake imewataka raia wa Afrika Kusini kumshika mkono kwa kuchangia fedha zitakazoweza kumsaidia kulipia gharama za wakili.

Ujumbe huo umeambatana na namba ya akaunti ikiwa na jina la JG Zuma;

Zuma anatumikia kifungo cha miezi 15-tangu aliposhtakiwa kwa kuidharau mahakama kwa kushindwa kufika mahakamani kusikiliza kesi dhidi yake kuhusu tuhuma za rushwa.

Zuma alikuwa amelazwa hospitalini mapema mwezi huu hivyo kuchelewesha kuanza kusikilizwa kwa kesi yake dhidi ya tuhuma za rushwa.

Anakabiliwa na kesi mbili ikiwa ni pamoja na ufisadi na ulaghai.

Zuma amekanusha tuhuma zote dhidi yake na kudai kuwa kesi hiyo ina ushawishi wa kisiasa.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...