Waziri Mkuu wa Israel, Naftali Bennett amekutana na Rais wa Marekani, Joe Biden siku moja baada ya shambulizi baya kwenye uwanja wa ndege wa Kabul uliosababisha vifo vya wanajeshi wa Marekani na raia wa Afghanistan.
Katika mkutano huo, Bennett alianza kwa kutoa salamu za pole kutokana na shambulizi hilo. Akizungumza na waandishi habari baada ya mkutano huo, Bennett amesema amefanikiwa katika malengo yake ikiwemo uhusiano kati ya nchi hizo mbili na suala la nyuklia ya Iran, katika ziara ya kwanza rasmi tangu achukue madaraka mwezi Juni.
Bennett amesema amekutana na kiongozi anayeipenda Israel, anayejua hasa kile anachokitaka na anayesikiliza mahitaji ya Waisraeli. Aidha, Biden amesema anatambua umuhimu wa kurekebisha hatua za kuimarisha maisha ya Wapalestina na kuwasaidia katika fursa za kiuchumi.
Biden amesema ana mtazamo sawa na Bennett na kwamba wamekuwa marafiki wa karibu.

No comments:
Post a Comment