Search This Blog

Saturday, August 28, 2021

Marekani yamuuwa aliyepanga shambulizi la Kabul


Jeshi la Marekani limesema limemuua mtu anayedaiwa kupanga shambulizi kwenye uwanja wa ndege wa Kabul katika shambulizi la ndege isiyo na rubani. Shambulizi hilo la jana lilimlenga mtuhumiwa wa kundi la wanamgambo linalofungamana na linalojiita Dola la Kiislamu, IS-K kwenye jimbo la Nangahar. 
 
Shambulizi hilo limefanyika baada ya Rais Joe Biden kuapa kupambana na IS baada ya shambulizi la juzi. Aidha, Marekani imesema itaendelea kuwaondoa raia wa Afghanistan kutoka uwanja wa ndege wa Kabul hadi dakika ya mwisho, licha ya kuwepo wasiwasi kuhusu mashambulizi kutoka kwa kundi la IS. 
 
Wizara ya Ulinzi ya Marekani imesema bado kuna vitisho vya kuaminika katika uwanja huo wa ndege. Marekani bado inaendelea na mchakato wa kuwaondoa raia wa Afghanistan wanaotaka kuondoka. Msemaji wa kundi la Taliban amesema kwamba wamechukua udhibiti wa maeneo ya uwanja wa ndege. Hata hivyo, Marekani imekanusha taarifa hizo.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...