Search This Blog

Tuesday, August 24, 2021

Wawakilishi wa wananchi wa Nyandoto watofautiana na halmashauri Mji wa Tarime


Na Timothy Itembe Mara.

Baadhi ya wawakilishi wa wananchi walikokuwa wameitwa ofisi ya halmashauri ya Mji wa Tarime kupokea maelekezo ya mgogoro wa Nyandoto wameshindwa kufikia mwafaka kutokana na kile kilichodaiwa kuwa  wanawashinikiza kununua viwanja badala ya kupimiwa walipie gharama za upimaji.
 
Akiongea Alani Okelo alisema anawashukuru watu wa halmashauri ya Mjiwa Tarime kuwaita ili kutatua mgogoro uliodumu kwa mda mrefu.
 
"Mmi niwapongeze watu wa halmashuri ya Mji wa Tarime kutuita kuja ili tutatue mgogoro wa Nyandoto lakini tunachosikia ni kile kile cha siku zote tunaomba maelekezo ya Naibu Waziri nyumba maendeleo na makazi aliyoyatoa Musoma juu ya mgogoro huu kwasababu tulikaa naye na akatusikiliza akasema nimewasikiliza nimegundua halmashauri walikuja kupima maeneo yenu bila kuwashirikisha sasa inakuwaje mrudie maelezo yenu yale yale ya kila siku ambayo tunalalamikia ambayo kila siku mnatupatia hakuna kipya tunaomba maelekezo kutoka kwa Naibu waziri aliyowapa"alisema Okelo.
 
Okelo alingeza kuwa mmetuondolea hadhi ya kuwa wamiliki licha ya kuwa Naibu waziri nyumba maendeleo na makzi,Angelina Mabula alitusikiliza na kugundua kuwa halmashauri ilipima viwanja kwenye maeno yetu bila kutushirikisha na kuwauzia wengine ambapo aliagiza kwa masiko yetu  turudishiwe maeneo yetu na tupimiwe viwanja kwa kushirikishwa kwa kutumia wataalamu wa Serikali na tulipie gharama za upimaji na tupewe nda wa kulipia na kwa atakaye  shindwa kulipia atanyanganywa  na halmashauri itaenda kumuuzia mwingine lakini tunachokutana nacho leo halmashauri ni kuwa tupimiwe na tulipie viwanja vilivyopimwa gharama za viwanja kama wengine walioomba sisi hilo hatutakubaliana.
 
Naye Butebi Moya alisema kuwa viongozi ndio mnaotuyumbisha na kuanzisha mgogoro maeneo niyetu tena inakuwaje mnatuambie kuwa tulipie gharama za kununua viwanja vyetu kama watu wengine tunaomba tupimiwe tulipie gharama za upimaji viwanja sio kunukunua viwanja ambavyo ni maeneo yetu.
 
Moya aliongeza kusema tunaomba Busara itumike katika hili kwa sababu mgogoro huu umedumu kwa mda mrefu nasisi tunaomba mgogoro ufike mwisho lakini kwa majibu haya tuliyoyasikia hatutafikia mwafaka kwasbabu halmashauri awali alikuwepo mkurugenzi Venuas Mwamengo alitusikiliza kilichokuwa kimebaki ni juu ya watu waliovamia maeneo yetu wakidai wanahati ili kukaa nao na kujua hatima,hatimaye akahamishwa sasa ofisi ipo haikuhama leo mnatwambia maeneo sio yakwetu na kuwa tunayamiliki kinyume cha sheria hatutakubali wengine tulizaliwa hapo na mababu zetu walizikwa hapo makaburi yao yapo.
 
Kwa upande wa kaimu mkurugenzi,Erasto Mbunga aliwasihi wawakilishi hao kukubali maelekezo waliopatiwa na viongozi wao kutoka ngazi za juu yakiwemo ya Kamishina wa ardhi mkoa Mara,mkuu wa mkoa Mara na Naibu waziri nyumba na maendeleo ya makazi ya kuwataka watume maombi ili kupatiwa viwanja na walipie kwa mda mwafaka kama wengine walivyoomba.
 
Kwa bahati nzuri mlifika kwa Naibu waziri nyumba maendeleo na makazi,Angelina Mabula alipokuwa Musoma kwenye ziara ya kikazi na pia mkaibuka kwenye mkutano wa mkuu wa mkoa Mara,Aly Happy ambapo Naibu Waziri alimwelekeza Kamishina wa ardhi na kamishina ametuelekeza kwa barua yake kukaa na nanyi ili kumaliza mgogoro kwa maelekezo ya kupimiwa viwanja na kulipia gahara kama wengine wanavyonunua kutoka halmashauri hiyo ni kutokana na kuwa maeneo mnayoyamiliki kwa sasa sio mali yeu ni mali ya halmashauri na mtapewa mda wa siku 90 kilipia na kila mtu aombe viwanja kulingana na uwezo alionao aliongeza kusema Mbunga.
 
Mwanasheria wa halmashauri,Haruna Matata alisema kuwa tumewaita hapa kwa maelekezo ya viongozi wetu waliotuelekeza kukaa na ninyi kutatua mgogoro kufuatia maelekezo ya mkuu wa mkoa kupitia mkutano wa wananchi uliofanyika tarehe 13/08/2021 pamoja na maelekezo ya Mh Naibu waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi aliyoyatoa tarehe 06/08/2021 Musoma kuhusu mgogoro wa eneo lililopimwa viwanja mtaa wa Nyagesese kama hamtakubaliana na hayo nendeni tu mahakamani.
 
Tunafahamu wananchi 122 wanalalamika licha ya kuwa hawana uhalali wa maeneo hayo tunaomba waombe maombi ya kupewa viwanja kama wengine wanavyoomba na watapewa kipaumbele kwanza alisema Matata.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...