
Wizara ya mambo ya nje ya Eritrea' imekataa vikwazo vilivyowekwa na Marekani dhidi ya mkuu wa jeshi ,na kuelezea kuwa havina msingi wowote.
Filipos Woldeyohannes alishukiwa kuwa kamanda mkuu wa jeshi la Tigray ambalo lilikiuka haki za binadamu.
Lakini Eritrea katika taarifa yake imeitaka Marekani kuja na vielelezo vitakavyothibitisha madai hayo ya uongo.
Wizara ya mambo ya nje imekiomba kitengo cha usalama cha Umoja wa mataifa kuingilia suala hili na kuhakikisha kuwa utawala wa nchi unaheshimiwa.
Chini ya vikwazo hivyo , Mali zote zinazomilikiwa na Jenerali Filipos zitazuiwa na biashara yeyote na Marekani imepigwa marufuku.
Marekani imetoa wito kwa Eritrea kuondoa majeshi yake nchini Ethiopia.
No comments:
Post a Comment