Search This Blog

Wednesday, August 11, 2021

Watu 42 wamefariki kutokana na moto uliotokea msituni, Algeria

 Watu wapatao 42 wamefariki kutokana na moto uliotokea katika maeneo zaidi ya 100 ya porini nchini Algeria.

Moto mkubwa zaidi umetokea katika maeneo ya milima katika mkoa wa Kabylie , ambapo wanajeshi 25 wamefariki wakati wakipambana kuzima moto huo.

Rais wa Algeria, Abdelmajid Tebboune ametuma salamu za rambirambi kwa familia za wahanga , amesema wanajeshi wameweza kuwaokoa watu zaidi ya 100 kutoka kwenye moto.

Waziri wa mambo ya ndani anawashuku kuwa wachomaji misitu wanahusika na janga hilo la moto.

Matukio ya moto katika eneo la pori katika mataifa ya ukanda wa Mediterranea yamezidi kutokana na joto kuongezeka na kiwango cha ukame kuongezeka.

Mji mkuu wa Tunisia, Tunis, umeshuhudia kiwango cha juu zaidi cha joto cha nyuzi joto 48C siku ya Jumanne.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...