Rais wa Marekani Joe Biden amesema hajutii maamuzi yake ya kuondoa majeshi kutoka Afghanistan, wakati Taliban ikiendelea na mapambano.
Bwana Biden amewataka viongozi wa Afghanistan kuwa na umoja na kupigania nchi yao.hasia zimeongezeka katika taifa hilo kwa sasa huku majeshi ya Marekani ambayo yalikuwa yanafanya operesheni zake kwa miaka 20 kuondoka.
Taliban imechukua maeneo nane ya miji mikubwa 34 ya taifa hilo na huku wakitishia miji mingine.
Akizungumza na waandishi wa Ikulu ya Marekani siku ya Jumanne, bwana Biden amesema Marekani ilikuwa inatimiza ahadi iliyoweka kwa Afghanistan, kama vile kusaidia katika anga, kuwalipa mishahara wanajeshi,pamoja na kuwapa chakula na vifaa wanajeshi.
Lakini alisema: "Wanapaswa kupigana wenyewe."
Zaidi ya raia 1,000 wameuawa katika mapigano kati ya Taliban na jeshi la serikali katika mwezi uliopita, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.
Huku wakala wa shirika linalohusiana na watoto, Unicef ikitoa angalizo wiki hii kuwa mauaji ya watoto yanaongezeka kila siku.

No comments:
Post a Comment