Search This Blog

Wednesday, August 11, 2021

Azm FC, Big Bullets vitani leo Kagame CUP


AZAM FC leo itakuwa na kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Big Bullets ya Malawi katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Kagame.

Ni majira ya saa 1:00 usiku, Uwanja wa Azam Complex mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kwa timu zote mbili kupambania nafasi ya kutinga hatua ya fainali.

Mshindi wa mchezo wa leo atakutana fainali na Express ambayo ilishinda nusu fainali ya kwanza Uwanja wa Azam Complex mbele ya KMKM kwa mabao 2-1.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo wa leo na wanahitaji ushindi ili kutinga hatua ya fainali.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...