Search This Blog

Monday, August 2, 2021

Watu 35 wafariki kwenye mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa nchini Niger

 Watu 35 wameripotiwa kupoteza maisha katika mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa nchini Niger.

Katika taarifa ya maandishi iliyotolewa na Taasisi ya Ulinzi wa Kiraia, iliripotiwa kuwa nyumba 2,500 zimekuwa chini ya maji tangu Juni kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa.

Katika taarifa hiyo, ilielezwa kuwa watu 26,532 waliathiriwa na mafuriko, watu 20 walipoteza maisha kwa kuwa chini ya majengo yaliyoanguka kutokana na mafuriko, na watu 15 walizama.

Mvua nchini Niger, ambayo hunyesha zaidi katika kipindi cha Juni-Septemba, husababisha mafuriko ya mara kwa mara.

Katika kipindi hicho mwaka jana, watu 73 walipoteza maisha katika mafuriko.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...