SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limeingia mkataba wa haki ya matangazo ya Ligi Kuu kwa upande wa Radio na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wenye thamani ya Sh bilioni 3.
Mkataba huo ambao umesainiwa leo Agosti 3,2021 ni wa muda wa miaka 10.
Mkataba huo umesainiwa baada ya kuwa na makubaliano kwa pande zote mbili ambapo Rais wa TFF, Wallace Karia aliweza kumwaga wino kwa ajili ya mkataba huo kwa upande wa TFF.
Ni Gabriel Nderumaki, Mratibu wa Masuala ya Masoko alikuwa ni mmoja ya wale waliosaini mkataba huo kwa upande wa TBC.
Karia amesema kuwa ni hatua nzuri ambayo wamefikia katika kusaini mkataba huo ambao utaongeza thamani ya soka la Tanzania pamoja na ubora wa ligi.

No comments:
Post a Comment