Search This Blog

Sunday, August 29, 2021

Rais Biden: Kuna uwezekano wa shambulio lingine Afghanistan

 


Rais wa Marekani, Joe Biden ameapa kuendeleza mashambulio ya angani dhidi ya kundi la itikadi kali nchini Afghanistan ambalo shambulio lake la kujitoa mhanga katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kabul lilisababisha vifo vya Waafghani na wanajeshi 13 wa Marekani. 

Baada ya kupokea taarifa kuhusu operesheni ya ndege zisizoendeshwa na rubani za Marekani katika eneo la mashariki mwa Afghanistan ambayo wizara ya ulinzi nchini humo imesema kuwa wanachama wawili wa tawi la kundi linalojiita dola la kiislamu IS nchini Afghanistan wameuawa, Biden alisema kundi hilo linapaswa kutarajia mashambulio zaidi. 

Katika taarifa, Biden amesema hilo halikuwa shambulio la mwisho na kwamba wataendelea kuwasaka watu wote waliohusika katika mauaji hayo na kuwachukulia hatua. 

Biden aliwapongeza wanajeshi wanaofanya shughuli ya kuwaondoa maelfu ya watu kutoka uwanja huo wa ndege wa Kabul kwa ushujaa na kujitolea kwao pamoja na kutuma salamu za rambirambi kwa mauaji ya wanajeshi 13 waliouawa katika shambulio uwanjani humo.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...