Search This Blog

Sunday, August 29, 2021

Viongozi Sudan Kusini wakubaliana mkataba wa muungano wa kijeshi

 


Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir amefikia makubaliano na aliyekuwa mpinzani wake Riek Machar yatakayotoa fursa ya kuungana kwa vikosi vyao pinzani. Haya yamesemwa jana na waziri wa masuala ya baraza la mawaziri Martin Elia Lomuru. 

Hatua hiyo ni ufanisi katika mchakato wa kutafuta amani nchini humo.Tangazo hilo la jana linaleta matumaini kwamba mchakato huo dhaifu wa amani utamaliza miaka mingi ya mvutano na kusababisha kuundwa kwa kikosi cha muungano, hili likiwa suala kuu katika mkataba wa amani wa mwaka 2018. 

Hata hivyo, katika ishara ya ukosefu wa uaminifu kati ya pande hizo mbili na uwezekano wa makubaliano yoyote kuvunjika, msemaji wa Machar, ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kwamba hakuna makubaliano yaliofikiwa.

Awali Lomuro aliwaambia wanahabari kwamba pande hizo zilikuwa zimekubaliana mpango wa kugawana madaraka ili kugawana udhibiti wa uongozi kusimamia usalama wa kitaifa.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...