Vikosi vya kundi laTaliban nchini Afghanistan vilifunga uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kabul jana kwa Waafghani wengi wanaotarajia kuhamishwa wakati ambapo Marekani na washirika wake wakikamilisha shughuli ya kuwaondoa watu itakayokamilisha miongo miwili ya uwepo wa vikosi vyao nchini Afghanistan.
Ijapokuwa washirika wengi wa Marekani wamekamilisha shughuli ya kuwaondoa watu, Marekani inapanga kuiendeleza hadi muda wa mwisho huku ikisema kuwa watu 113,500 wamehamishwa tangu Agosti 14 siku moja kabla ya kundi la Taliban kuchukuwa uongozi wa taifa hilo.
Biden ameonya kuwa makamanda wa kijeshi wamemuarifu kuna uwezakano wa kutokea shambulio lingine katika muda wa saa 24-36.
Viongozi wa Magharibi wamekiri kwamba kujitoa kwao kutamaanisha kuwaacha baadhi ya raia wao na wenyeji wengi ambao waliwasaidia kwa muda mrefu nchini humo na kuapa kuendelea kushirikiana na kundi hilo la Taliban kuwaruhusu washirika wao nchini humo kuondoka baada ya kumalizika kwa muda wa mwisho wa Rais Biden wa kuondoka nchini humo.

No comments:
Post a Comment