Search This Blog

Thursday, August 5, 2021

Mtandao wakwamisha kesi ya Mbowe


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam imeshindwa kusikiliza kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake watatu kutokana na uhafifu wa mtandao.

Akizungumza na waandishi wahabari Mahakamani hapo mara baada ya kutoka katika kesi hiyo, Wakili wakili wa Mbowe Peter Kibatala amesema shauri hilo la Uhujumu uchumi lenye mashitaka ya ugaidi litasikilizwa kesho saa tatu asubuhi huku watuhumiwa Mbowe na wenzake wakitarajiwa kufika Mahakamani hapo.

Kibatala amesema, kesi hiyo iliyosikilizwa kwa njia ya mtandao baada ya uamuzi wa mahakama kutokana na sababu zilizotajwa ikiwemo ugonjwa wa Corona, hivyo pande zote mbili zikakubaliana kusikiliza kesi hiyo kwanjia ya mtandao (Video conference) lakini kwa bahati mbaya teknolojia imefeli kutokana na mawasiliano hafifu kati ya Mahakama ya kisutu na Gereza la ukonga.

Kwa mara ya kwanza, Mbowe alifikishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kusomewa mashitaka yake Julai 26, 2021.


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...