Search This Blog

Thursday, August 5, 2021

Manyara yaanza kutoa chanjo ya corona kwenye vituo 21


Na John Walter-Manyara

Mkoa wa Manyara umepokea dozi 15,000 ya chanjo ya ugonjwa wa Uviko-19 kwa awamu ya kwanza na kusambazwa katika Halmashauri zote saba za mkoa huo.

Akitoa taarifa kwa wananchi kupitia kwa waandishi wa habari, Mganga mkuu wa mkoa wa Manyara Dr. Damas Kayera amesema chanjo imeshaanza kutolewa  kwa makundi maalumu wakiwemo wale wenye magonjwa sugu kuanzia umri wa miaka 18 na kuendelea, watu wenye umri mkubwa kunzia miaka 45, na watumishi wa afya ambapo kuna jumla ya vituo 21.

Amewataka wananchi wote kujitokeza kwa wingi ili kupatiwa chanjo hiyo kwa lengo la kujikinga na ugonjwa wa Corona ambao umekuwa tishio Duniani.

Dr. Kayera  amesema kila Halmashauri wametenga vituo vitatu ambapo katika wilaya ya Mbulu watu watapata huduma ya kuchanja katika hospitali ya wilaya ya Mbulu, Daudi na Gehandu huku halmashauri ya Mbulu vijijini ni Hydom,Dongobesh na Muslu.

Babati mjini ni Hospitali ya mkoa,Hospitali ya mji Mrara na Kituo cha Afya Bonga wakati Babati Vijijini ni Dareda,Magugu na kituo cha Afya Galapo.

Wilaya ya Hanang wananchi watapata chanjo katika Hospitali ya Tumaini,Katesh na Endasak.

Katika wilaya ya Kiteto ni Kibaya,Sunya na  Engusero huku wilaya ya Simanjiro wakipata huduma katika vituo vya Mererani,Orkeset Arban pamoja na Naberera.

Amewatoa hofu wananchi kwa kuwaeleza wenye nia ya kuchanja wajitokeze kwa sababu ni salama wataalamu wa afya wamethibitisha kuwa haina madhara yeyote na kuwasisitiz waendele kuchukua tahadhari zote zinazoelekezwa na wataalamu wa afya.

Amesema kupata huduma hiyo lazima uwe na kitambulisho kinachotambulika kama cha mpiga kura au cha Taifa.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...