Mahakama ya juu kabisa ya Brazil imeamuru rais wa nchi hiyo Jair Bolsonaro achunguzwe kwa madai ambayo hayajathibitishwa kwamba mfumo wa kupigia kura wa Brazil unagubikwa na udanganyifu.
Hukumu iliyotolewa na jaji Alexandre de Moraes imetolewa baada ya Bolsonaro kuongeza ukosoaji wake kwa mfumo wa kupiga kura kwa njia ya kielektroniki akisisitiza hakutafanyika uchaguzi mwaka ujao kama ilivyopangwa ikiwa hakutafanyika mageuzi.
Mfumo huo ulianzishwa mnamo 1996. Bolsonaro amesema uchunguzi dhidi yake uko nje ya mipaka ya katiba na ametishia kuchukua hatua nje ya katiba bila kufafanua.

No comments:
Post a Comment