Mpinzani mkubwa wa Rais wa Urusi, Alexei Navalny ametembelewa na mke wake, Yulia Navalnaya kwa mara ya kwanza, ambapo ameruhusiwa pia kubaki katika gerezani hilo kwa siku tatu.
Navalnaya mwenye umri wa miaka 45, pamoja na kuonesha picha yake, ameandika kwenye ukurasa wake wa instagram kwamba ametumia kiasi fulani cha muda katika gereza la Pokrov, ambalo lipo umbali wa kilometa 100 mashariki wa jiji la Moscow.
Navalny ambae pia ana umri wa miaka 45 amekutwa na na mikasa ya vifungo vya mara kwa mara. Alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Moscow katikati ya Januari wakati akirejea nchini Urusi akitokea Ujerumani.
Kifungo chake kinatokana na kile kinachodaiwa kuvuruga ripoti ya mashtaka yake ya jinai ya awali, wakati akipatiwa matibabu nchini Ujerumani baada ya jaribo la kuuwawa kwa kutimia simu aina ya Novichok.

No comments:
Post a Comment