Wizara ya mambo ya nje ya Uganda imekanusha kuwa na rekodi ya safari iliyozuiwa ya Naibu rais wa Kenya nchini humo.
Waziri Okello Oryem amesema kuwa ofisi yake haikupokea ombi loloto la itifaki kwa Bw William Ruto.
Amesema kuwa hakujulishwa kuhusu ziara yake nchini Uganda.
Bw Ruto alikuwa amesema kuwa alikuwa anataka kuizuru Uganda kwa masuala yake ya kibinafsi.
Kipindi cha nyuma aliitembelea Uganda na kupiga picha na Rais Yoweri Museveni akizundua mradi.
Jumatatu Bw Ruto alizuiwa kusafiri kwa ndege nje ya nchi na maafisa wa uhamiaji wakisema kuwa alihitaji idhini kutoka kwa rais.
Hatahivyo naibu huyo wa rais amepuuzilia mbali kigezo hicho cha kumzuia kwenda nje ya nchi akisema kuwa amewahi kusafiri nje ya nchi siku zilizopita na hakuwahi kuzuiwa kwasababu ya idhini ya rais.
Alisema kuwa suala hilo limetokana na "mapambano ya mamlaka ya vyeo" ya chama tawala.
Waziri wa Uganda Oryem amesema kuwa nchi yake haiingilii katika masuala ya ndani ya nchi yoyote kwa vyovyote vile.
"Hatuna mamlaka, hatuna nguvu juu ya serikali ya Kenya, wana sababu zao wenyewe za kumzuia Ruto kuja Uganda… na suala hilo linapaswa kupelekwa katika ubalozi wa Kenya," alisema.

No comments:
Post a Comment