Search This Blog

Sunday, August 1, 2021

Marekani yamshinikiza rais wa Tunisia kurejea katika njia ya kidemokrasia

 


Mshauri wa usalama wa kitaifa wa Marekani Jake Sullivan, amemuhimza rais wa Tunisia Kais Saied kutoa muongozo wa kurejea katika njia ya kidemokrasia kufuatia hatua yake ya kuchukuwa udhibiti wa taifa hilo Jumapili iliyopita. 

Haya ni kwa mujibu wa ikulu ya White House. Katika taarifa, baraza la usalama la ikulu hiyo ya White House limesema kuwa kupitia mazungumzo kwa njia ya simu, Sullivan alimsisitizia Saied haja ya kuunda serikali mpya kwa haraka itakayoongozwa na waziri mkuu mwenye uwezo itakayoimarisha uchumi wa taifa hilo na kukabiliana na janga la virusi vya corona pamoja na kuhakikisha kurejea kwa wakati kwa bunge lililochaguliwa.

Rais Saied alitaja kuwa dharura ya kitaifa janga la virusi vya corona na uongozi mbaya na kumuondoa waziri mkuu, kusitisha shughuli za bunge na kuchukuwa udhibiti wa taifa hilo katika hatua iliyopongezwa na wananchi huku wapinzani wake wakiitaja kuwa mapinduzi.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...