Search This Blog

Monday, August 23, 2021

Kesi ya Mbowe kuendelea leo


Kesi namba 63/2020 ya Uhujumu Uchumi inayomkabili, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) inaendelea katika Mahakma ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo Agosti 23, 2021.

Kesi hiyo yenye mashtaka ya Ugaidi, imeitwa leo chini ya hati ya dharura mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu ,Thomas Simba ambapo Agosti 13 mwaka huu kesi hiyo iliahirishwa hadi Agosti 27.

Hatua hiyo ni baada ya Mwendesha Mashtaka wa serikali (DPP) kuwasilisha hati ya Mashtaka na Ushahidi katika Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salam ambayo imesajiliwa kama kesi ya uhujumu uchumi namba 16/2021.


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...