Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima amefika kuhojiwa katika Kamati ya Bunge haki, maadili na madaraka ya Bunge leo mchana.
Gwajima amefika saa 6.36 mchana akiwa katika gari nyeusi.
Alipofika katika geti kubwa linalotumiwa na wabunge bungeni , alipokelewa na askari wawili mmoja akiwa amevalia nguo za Polisi na mwingine nguo za kiraia.
Askofu Gwajima akiwa ameongoza na askari hao alielekezwa kukaa katika viti vilivyoko baada ya mashine ya kukagua iliyoko katika jengo la utawala akisubiri kuitwa ukumbi
No comments:
Post a Comment