Jeshi la Israel limesema kuwa limeshambulia kwa mabomu maeneo ya silaha ya wapiganaji wa Palestina katika ukanda wa Gaza mapema leo kujibu maandamano ya vurugu kwenye ukuta unaotenganisha Israel na ukanda huo yaliyosababisha kujeruhiwa kwa afisa mmoja wa polisi wa Israeli.
Vurugu za jana ziliibuka baada ya mamia ya Wapalestina kufanya maandamano yaliyoandaliwa na viongozi wa kundi la Hamas katika ukanda wa Gaza kulalamikia kuzingirwa kwa Uganda wa Gaza kunakofanywa na Israeli pamoja na Misri.
Maandamano hayo yaliongezeka kuwa makubwa baada ya mamia ya watu kufika katika ukuta huo wa mpakani na kurusha mawe na vilipuzi kuelekea kwa wanajeshi wa Israeli.
Kwa mujibu wa wizara ya afya katika eneo la Gaza, kiasi cha Wapalestina 24 ikiwa ni pamoja na mtoto wa umri wa miaka 13 walijeruhiwa kutokana na ufyetuaji risasi kutoka kwa jeshi la Israeli.

No comments:
Post a Comment