Makamu rais wa Marekani Kamala Harris leo ameanza ziara yake ya bara Asia ambapo ataelezea kujitolea kwa Marekani katika kanda hiyo baada ya kuondolewa kwa vikosi vyake nchini Afghanistan na kundi la Taliban kuchukuwa uongozi.
Lakini katika ziara yake itakayomfikisha nchini Singapore na Vietnam, Harris atatafuta kuondoa wasiwasi kuhusu kutegemewa kwa Marekani.
Ziara hiyo ya Vietnam imeibua ukosoaji huku baadhi ya watu wakimshtumu Harris kwa kuzuru taifa hilo wakati vikosi vya Marekani vinajizatiti kuwaondoa raia wa Marekani, wengine wa kigeni na washirika wake wa Afghanistan kutoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kabul.
Hata hivyo, maafisa wa Marekani wanasema kuwa ziara hiyo ilikuwa imepangwa muda kabla ya mzozo huo wa Afghanistan na kusisitiza kuwa Harris anazingatia malengo makubwa ya kimkakati barani Asia.

No comments:
Post a Comment