Search This Blog

Sunday, August 22, 2021

Raia 7 wa Afghanistan wauawa katika uwanja wa ndege wa Kabul

 


Vurugu katika uwanja wa kimataifa wa ndege mjini Kabul nchini Afghanistan, zimesababisha vifo vya raia wengine saba wa nchi hiyo. 

Jeshi la Uingereza limesema haya leo na kuonesha hatari inayowakabili wale ambao bado wanajaribu kutoroka utawala wa Taliban nchini humo. 

Vifo hivyo vimetokea huku kile kinachoonekana kuwa tishio jipya la tawi la kundi la itikadi kali linalojiita dola la Kiislamu IS nchini Afghanistan likisababisha ndege za kivita za Marekani kutua kwa haraka katika uwanja huo wa ndege uliozingirwa na wapiganaji wa Taliban. 

Ndege nyingine zimerusha mioto wakati wa kupaa katika juhudi za kuyachanganya makombora yanayotafuta joto yanayozilenga ndege hizo.

Mabadiliko hayo yanafanyika wakati ambapo ubalozi wa Marekani jana ukitoa onyo jipya la usalama kwa raia kutokwenda katika uwanja wa ndege wa Kabul bila ya maagizo binafsi kutoka kwa mwakilishi wa serikali ya Marekani.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...