Search This Blog

Sunday, August 8, 2021

Iran iko tayari kurudi tena kwenye mazungumzo ya nyuklia

 


Iran imesema iko tayari kufufua mazungumzo ya makubaliano ya nyuklia pamoja na mataifa yenye nguvu ulimwenguni chini ya uongozi wa rais mpya Ebrahim Raisi. 

Halikadhalika maafisa wa Umoja wa Ulaya wamesema kwamba mazungumzo yanaweza kuanza mwanzoni mwa mwezi Septemba mjini Vienna, Austria. 

Afisa anaetarajiwa kusimamia mazungumzo hayo kwa upande wa Umoja wa Ulaya Enrique Mora, alihudhuria kuapishwa kwa Raisi mjini Tehran siku ya Alhamisi. 

Akiwa huko alizungumza na afisa wa Iran aliyeteuliwa kusimamia mazungumzo ya nyuklia, Hossein Amir-Abdollahian. 

Aidha kuna fununu kwamba huenda Amir-Abdollahian akateuliwa kama waziri mpya wa mambo ya nje kwenye baraza la mawaziri la Raisi.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...