Maelfu ya watu wameyahama makazi yao katika kisiwa cha Ugiriki cha Evia wakati moto wa msituni ukiwa unaendelea kuwaka kwa siku ya sita mfululizo.
Maferi yamekuwa yakifanya kazi ya kuwavukisha watu baharini na kuwapeleka kwenye maeneo salama.
Moto huo ambao ulitishia kuteketeza vitongoji vya kaskazini mwa mji mkuu wa Athens ulififia siku za hivi karibuni.
Lakini badala yake ulizuka katika kisiwa kikubwa cha Evia mashariki mwa mji huo, chenye maelfu ya hekta za msitu katika upande wake wa kaskazini.
Serikali ya Ugiriki imepeleka wanajeshi kusaidia kupambana na moto huo.
Aidha nchi kadhaa zikiwemo Ufaransa, Misri, Uswizi na Uhispania pia zimetuma msaada ikiwa ni pamoja na ndege za kuzimia moto.

No comments:
Post a Comment