Search This Blog

Wednesday, August 25, 2021

Bunge la Iran laidhinisha wateule wa baraza la mawaziri

Bunge la Iran limepiga kura na kuyaidhinisha karibu majina yote ya baraza la mawaziri aliyoyateua Rais Ebrahim Raisi.

Baraza hilo la mawaziri hata hivyo, halikuwa na mwanamke hata mmoja japo walikuwepo maafisa kadhaa kutoka kikosi cha ulinzi cha mapinduzi cha Iran.

Kati ya mawaziri 19, bunge la Iran limeidhinisha majina ya mawaziri 18 walioteuliwa kwa nafasi za uwaziri na kiongozi huyo mhafidhina mwenye msimamo mkali.

Hata hivyo, bunge hilo lilikataa jina la waziri aliyeteuliwa kuongoza wizara ya elimu, na kumlazimu Rais huyo kumteua mtu mwengine.

Bunge la Iran halikumkubali Hossein Baghgoli, ambaye uzoefu wake ulitiliwa mashaka.

Raisi alikuwa amelihimiza bunge kupiga kura haraka na kuidhinisha wateule wake katika nafasi za uwaziri ili serikali yake ianze kufanya kazi mara moja kushughulikia mlima wa changamoto zinazoikabili nchi hiyo ya Mashariki ya kati.

"Mpango wetu ni kuchagua njia bora za ushirikiano na nchi nyengine. Utu, hekima na uadilifu ni nguzo muhimu za kufanikisha majukumu yetu pamoja na kutimizia maslahi mapana na haki za taifa letu."

Raisi mwenye umri wa miaka 60, anachukuwa madaraka katika wakati ambapo Iran inakabiliwa na hali ngumu ya kiuchumi na kijamii.

Iran inapitia kipindi kigumu kutokana na vikwazo iliyowekewa na Marekani baada ya Rais wa zamani Donald Trump kujiondoa kwenye makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2018.

 Baraza hilo la mawaziri halina mwanamke hata mmoja

Rais huyo mpya aliapishwa na bunge mapema mwezi Agosti, lakini utawala uliomaliza muda wake ulisalia madarakani hadi siku ya Jumatano baada ya kura ya bunge.

Waziri mpya wa mambo ya nje Hossein Amirab-dollahian amesema wizara yake, haitaikimbia meza ya mazungumzo na kwamba wizara hiyo itafanya kila iwezekanalo kuondoa vikwazo vyote dhidi ya nchi hiyo.

Amirab-dollahian mwenye umri wa miaka 56 ana uzoefu mkubwa baada ya kuhudumu katika nyadhifa mbalimbali za uongozi serikalini kwa miaka kadhaa.

Kwa mshangao wa wengi, baraza hilo la mawaziri halikuwa na mwanamke hata mmoja.

Mnamo siku ya Jumamosi, Rais huyo wa Iran alisema kipaumbele cha kwanza cha serikali yake ni kupambana na janga la virusi vya Corona kabla ya kulekeza nguvu zake katika kuufufua uchumi.

Mataifa ya Magharibi, ikiwemo Urusi na China zinaangalia kwa jicho la karibu ishara zozote za Iran kuanza tena mazungumzo ya Vienna yanayolenga kuunusuru mkataba wa mpango wa nyuklia wa Iran.

 

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...