Poland imesitisha shughuli ya uhamishaji kutoka mji mkuu wa Afghanistan wa Kabul, kwa sababu za usalama.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland Marcin Przydacz alisema kuwa baada ya Taliban kuchukua udhibiti wa Kabul mnamo Agosti 15, uhamishaji wa wale ambao walitaka kuondoka Afghanistan kutoka uwanja wa ndege wa Kabul ulisimamishwa kwa sababu za usalama.
Przydacz alisisitiza kuwa kundi lililohamishwa kutoka Kabul na kwa sasa lililoko Uzbekistan ndio kundi la mwisho la uhamishaji kwa Poland.
Akitoa taarifa kwamba uamuzi huo ulichukuliwa baada ya kushauriana na Marekani na maafisa wa Uingereza, Przydacz alisema,
"Baada ya uchambuzi wa muda mrefu wa ripoti juu ya hali ya usalama, hatuwezi tena kuhatarisha maisha ya wanadiplomasia wetu na wanajeshi."
Uamuzi wa Poland ulikuja baada ya Rais wa Marekani Joe Biden kutangaza kuwa atasitisha safari za uhamishaji kutoka Kabul mnamo Agosti 31.
No comments:
Post a Comment