Search This Blog

Friday, August 27, 2021

Barnier kugombea urais Ufaransa


Aliyekuwa kamishna wa Umoja wa Ulaya na kiongozi wa mazungumzo ya Uingereza kwenye mchakato wa Brexit, Michel Barnier, ametangaza kuwa anapanga kugombea urais nchini Ufaransa kupitia chama cha Republican katika uchaguzi utakaofanyika mwakani. 
 
Barnier ametangaza hayo jana jioni kupitia televisheni ya TF1. Amesema kuna changamoto zinazowakabili katika nyakati muhimu, hivyo anatamani kuwa rais atakayeipatanisha Ufaransa. Mwezi Januari Barnier aliteuliwa kuwa mshauri muhimu wa Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen. 
 
Mwezi Desemba mwaka uliopita, alitangaza nia yake ya kurejea kwenye siasa za Ufaransa. Kabla ya kuhamia Brussels, Barnier alikuwa waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...