Mwendesha mashtaka wa nchini Algeria ametaka mwanaume anayeshukiwa kuwasha moto msituni kuchunguzwa.
Djamel Bensmail alifariki baada ya kupigwa na kuchomwa moto.
Tukio hili lilitokea eneo la Tizi Ouzou la taifa hilo ambapo eneo kubwa limeathirika zaidi na moto kwa siku kadhaa - na kuua watu wapatao 73.
Maelfu ya waombolezaji waliohudhuria msiba wa bwana Bensmail ambaye wazazi wake walisema alienda kusaidia kuzima moto.
Rais wa Algeria, Abdelmadjid Tebboune alisema washukiwa 22 waliodhaniwa kuwasha moto wamekamatwa.
Ndege mbili za Canada za kuzima moto zilizotumwa na Ufaransa zilijumuika katika jitihada za kuzima moto.
Ndege nyingine mbili ziliwasili kutoka Spain siku ya Ijumaa.

No comments:
Post a Comment