Search This Blog

Friday, August 13, 2021

Hatimaye Baba yake Britney Spears akubali kuacha kudhibiti mali za mwanae

 Baba yake Britney Spears amekubali kuacha jukumu la kudhibiti mali za binti yake baada ya miaka 13, taarifa za vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti.

Tasnia ya mwimbaji huyo imekuwa mikononi mwa wasimamizi wa kisheria baada ya umma kutoa wasiwasi wao juu ya afya yake ya akili mnamo mwaka 2008.

Mahakama ilitoa agizo kwa kumpa baba yake mwimbaji huyo bwana Jamie Spears, kudhibiti mali za mwanae.

Lakini baadae mwanamuziki huyo alifikiria kumuondoa baba yake katika jukumu hilo na kutaka ashtakiwe kwa kutumia vibaya mali zake.

Mara zote, Jamie Spears amekuwa akikanusha madai hayo na kueleza wasiwasi wake juu ya hali ya mwanae.

Huku kampeni ya kupinga udhibiti wa mali ya Britney ilianzishwa na baadhi ya mashabiki na kuitwa #FreeBritney, ambapo wanaamini kuwa maisha ya mwanamuziki huyo na taaluma yake yanadhibitiwa kinyume na matakwa yake.

Mwaka huu, kesi hiyo ambayo ilikuwa inachukua muda ilipata sura mpya baada ya kuzinduliwa kwa Makala ya Framing Britney Spears ambayo imeangazia mzozo wa usimamizi wa mwimbaji.

Mwanamuziki huyo mwenye miaka 39, alimwambia hakimu kuwa akilazimishwa kufanya maonesho bila ridhaa yake na kuzuiwa kuwa na watoto.

Usimamizi wa kisheria wa Spears umegawanyika katika sehemu mbili – upande mmoja ni kwenye nyumba zake na masuala ya kifedha,na upande mwingine ni kwake kama mtu.

Mwaka 2019, baba yake alijiondoa katika usimamizi wa masuala binafsi ya binti yake kutokana na masuala ya kiafya lakini mwimbaji huyo aliandika barua kuomba baba yake aondolewe kwenye udhibiti wa mali zake. Baadae akasema hataimba kwenye majukwaa tena kama baba yake ataendelea kubaki katika jukumu hilo la udhibiti wa mali zake.

Akijibiwa maombi yake, wakili wa bwana Spears alisema siku ya Alhamisi kuwa nakala za mahakama hazitoi muongozo wa kujiondoa.

Wakati wakili wa mwanamuziki huyo , Mathew Rosengart, alitoa taarifa inayosema: "Huu ni ushindi mkubwa kwa Britney Spears nah ii ni hatua nyingine katika kupata haki."



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...