Na Ezekiel Mtonyole, Arusha.
Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia itatumia zaidi ya shilingi Bilioni 2.1 kukarabati majengo na kujenga bweni jipya la wasichana katika Chuo cha Ufundi Arusha bweni litakalokuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi mia nne na ishirini(420) pindi litakapo kamilika ujenzi wake.
Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji ya Chuo hicho,Kaimu Mkuu wa Chuo hicho ,Dkt Yusuph Mhando amesema chuo hicho kilianzishwa mwaka 1978 kwa madhumuni ya kutoa mafunzo ya ufundi sanifu katika ngazi ya Cheti(Full Technician Certificate - FTC) ili kupata wataalamu wenye sifa na ujuzi katika fani mbalimbali za Ufundi.
Amesema Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia umefanya maboresho makubwa katika ukarabati wa Chuo hicho katika miondombinu ya chuo hicho pamoja na kuwekeza vifaa vya kisasa katika uendeshaji wa chuo hicho ili kutoa ujuzi bora.
Dkt Mhando anasema Chuo cha Ufundi Arusha kilipandishwa hadhi ya kiuendeshaji kupitia Gazeti la Serikali No. 78 la mwaka 2007 na kufanyiwa marekebisho kupitia Gazeti la Serikali Na. 302 la mwaka 2015.
Amesema ATC inatoa mafunzo ya ufundi stadi katika ngazi mbalimbali (level I, II na III) na elimu ya ufundi kwa ngazi za Astashahada, Stashahada na Shahada katika fani mbalimbali katika michepuo ya Sayansi, Teknolojia na Ufundi.
Kaimu Mkuu huyo amasema chuo hicho kinachoongoza kwa kutoa Mafunzo, Tafiti na Ushauri wa Kitaalamu vinavyoaendana na mahitaji ya soko kwa kutumia Sayansi, Teknolojia na ubunifu kwa maendeleo endelevu.
Amesema programu zinazoendeshwa chuoni hapo zimeanzishwa kwa kuzingatia, Sera za Taifa,Soko la ajira,Azimio la Kilimo Kwanza,upungufu wa mafundi wa Maabara za Sayansi katika Shule za Sekondari,Uharibifu wa vifaa tiba hospitalini,Mabadiliko ya teknolojia na utandawazi na teknolojia ya habari na mawasiliano.
Kaimu Mkuu huyo amesema chuo kinatoa Programu za kitaaluma 21 zinazotambuliwa na NACTE na kupewa ithibati.
Kaimu Mkuu huyo amebainisha kuwa kati ya fedha kiasi cha zaidi ya bilioni 2.1, Chuo kilipokea jumla ya shilingi bilioni 1.499 14/05/2021 kama ruzuku kutoka serikalini kwa ajili ya ujenzi wa bweni la wasichana lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 420.
“Mradi ulianza mwishoni mwa mwezi Mei, 2021 ambapo utekelezaji umefikia 15% na upo katika hatua za ujenzi wa msingi (substructure),”amesema.
Kaimu huyo Mkuu wa Chuo amesema ili kuwapatia wanafunzi na watumishi huduma za afya na kwa haraka chuo kilianza ujenzi wa kliniki kwa kutumia mapato yake ya ndani amesema Mradi ulianza mwishoni mwa mwezi Aprili, 2021 ambapo utekelezaji umefikia 30% na upo katika hatua za ujenzi wa msingi mkubwa (superstructure-framed structure)
Amesema mradi wa East Africa for Transformation and Regional Integration Project (EASTRIP)’ inalenga uanzishwaji wa Kituo cha Umahiri cha Kikanda katika Nishati Jadidifu.
Amesema thamani ya mradi ni Shilingi 37.4 billion , ambapo Chuo kimeshapokea shilingi 11.2 billion ambayo ni 30% ya fedha yote ya mradi kama kianzio.
Amesema IEEP ni mradi unaofadhiliwa na Wizara ya elimu ya Korea ambapo Mradi huo una thamani ya Shilingi bilioni tano kwa kipindi cha miaka saba kuanzia Aprili 2020 mpaka Machi 2027.
Amesema ATC inashirikiana na vyuo viwili vya Korea -Hanyang University na Seoul National University katika kutekeleza mradi huo.
Baadhi ya majengo yaliyofanyiwa ukarabati ni madarasa, hostel za wavulana na wasichana, na ujenzi wa tanki kubwa la maji lenye ujazo wa lita milioni 1.2 lililogharimu zaidi ya milioni mia mbili ambapo inafanya kufikia kiasi cha zaidi ya milioni mia saba(700) katika ukarabati wa miondombinu na ujenzi wa tanki la maji.
Mbali na ukarabati wa majengo serikali imewekeza vifaa vya kisasa na mitambo mipya ya mafunzo kwa wanafunzi ndani ya chuo hicho na kurahisisha ujifunzaji kwa wanafunzi.
Kwa upande wake mwanafunzi wa mwaka wa kwanza katika chuo hicho,anaesomea Electrical Biometrical Engineering, Wema Laurence amesema maboresho yaliyofanywa na Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia yatawasaidia kwa kiasi kikubwa katika masomo yao kwani watafika chuo kwa wakati kutokana na kukaa hosteli ambazo zipo karibu na Chuo.
“Tunaishukuru Serikali wameanza kutujengea hosteli mpya ambazo zitatuwewezasha sisi kufika darasani kwa wakati, ambao tulikuwa tunakaa nje tunapata changamoto za usafiri tunachelewa kufika sasa hivi tutakuwa tunafika kwa wakati,”amesema.
Kuhusiana na kusoma masomo ya umeme,anasema ndoto zake zilikuwa kuja kuwa mhandisi hivyo alivyofika chuoni hapo na msukumo wake ulikuwa katika masomo ya Sayansi alimua kujiunga na kozi ya umeme.
“Mimi nilikuwa napenda umeme na nilivyokuja hapa chuo nikakutana na Biometical nikaelezewa jinsi ilivyo na walionitangulia nikaipenda nikaamua kuingia kwenye Biometical,”amesema
|
08:11 (1 hour ago) |
||
|
|||


No comments:
Post a Comment