Search This Blog

Saturday, July 17, 2021

Waziri Mkuu wa Ubelgiji asema maafa ya mafuriko hayakutarjiwa


Waziri Mkuu wa Ubelgiji Alexander De Croo amesema mafuriko makubwa yaliyoikumba nchi hiyo ni mabaya zaidi katika historia na yameleta maafa ambayo hayakutarajiwa. 

De Croo ametoa matamshi hayo wakati akizungumzia athari za mafuriko zilizoikumba Ubelgiji na mataifa mengine ya Ulaya Magharibi ambayo yamesababisha vifo vya mamia ya watu na uharibifu mkubwa wa mali na miundombinu.

 Serikali ya Ubelgiji imetangaza Julai 20 kuwa siku ya maombolezo ya taifa kuwakumbuka watu 20 waliopoteza maisha katika mafuriko yaliyotokea katikati mwa wiki huku juhudi za kuwatafuta makumi wengine zikiwa zinaendelea.

Hadi jana jioni zaidi ya watu 126 wamekufa kwenye mataifa ya Ulaya kutokana mafuriko hayo na idadi kubwa zaidi imeripotiwa nchini Ujerumani ambako juhudi za uokozi zinaendelea huku mamlaka zikisema maelfu ya watu bado hawajapatikana .



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...