Polisi wa Haiti walikana madai kwamba maafisa wa serikali walihusika katika mauaji ya Rais Jovenel Moise.
Mkuu wa Polisi wa Haiti Leon Charles alitoa maelezo kwa waandishi wa habari wa Colombia kuwa madai ya kwamba waziri mkuu wa mpito Claude Joseph ndiye mtu aliyehusika na mauaji ya Moise hayana ukweli wowote.
Charles alisema hakuna ushahidi wa kuunga mkono madai hayo.
Kituo cha runinga kilichoko Colombia kilidai kwamba waziri mkuu wa mpito Joseph alikuwa nyuma ya mauaji ya Moise, kulingana na vyanzo vya Ofisi ya Upelelezi ya Marekani (FBI).
Moise alitangaza siku mbili kabla ya mauaji kwamba alikuwa amemteua waziri mkuu mpya kuchukua nafasi ya Joseph.
Charles alisema kuwa watu 23, pamoja na wanajeshi 18 wa zamani wa Colombia, walizuiliwa kuhusiana na mauaji hayo, na kwamba walipokea msaada kutoka kwa vitengo vya ujasusi vya nchi zingine, pamoja na FBI, katika upeo wa uchunguzi.
Kwa upande mwingine, Rais wa Marekani Joe Biden alisema kuwa kutuma wanajeshi Haiti sio ajenda yao.
Rais Moise mwenye umri wa miaka 53 aliuawa kwenye shambulizi la watu wenye silaha nyumbani kwake mnamo Julai 7, na mkewe, Martine Moise, alijeruhiwa.
Katika upeo wa operesheni, washukiwa 10 ambao walikabiliana na polisi waliuawa.

No comments:
Post a Comment