Search This Blog

Tuesday, July 27, 2021

Utapiamlo wa watoto kuongezeka mara nne Madagascar - UN



Mfuko wa chakula wa Umoja wa Mataifa umetahadharisha kuwa watoto nusu milioni kusini mwa Madagascar watakabiliwa na utapiamlo mkali.

Hii itakuwa ongezeko mara nne tangu tathmini ya awali iliyofanywa mnamo Oktoba 2020, WFP na shirika la watoto la UN, Unicef, yameshema Umoja wa Mataifa umesema mvua kidogo iliyonyesha kwa miaka mitano imesababisha upatikanaji wa chakula kuwa hafifu kwa wengi katika maeneo yaliyoathirika zaidi.

Robo tatu ya idadi ya watu wameathiriwa na kile kinachoelezewa kama janga baya la ukame na maambukizi ya Covid-19, yaliyosababishwa na ukosefu wa vifaa vya usafi wa mazingira na ukosefu wa maji salama ya kunywa.

"Kinachotokea hivi sasa kusini mwa Madagascar ni cha kusikitisha," alisema Moumini Ouedraogo, mwakilishi wa WFP nchini humo.

Afisa wa Unicef ​​wa eneo hilo alisema kuna hitaji la dharura la kushughulikia hali hiyo "kuzuia hali hiyo kuwa mbaya zaidi".

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...