Search This Blog

Tuesday, July 27, 2021

Jeff Bezos ajitolea kuilipa Nasa dola bilioni 2 kuzingatiwa kwa mradi wa safari ya kwenda mwezi

 

eff Bezos amejitolea kulipia $ 2bn (£ 1.4bn) ya gharama za Nasa ili kuzingatiwa tena kwa kandarasi muhimu ya kutengeneza chombo kitakachotumika kwenda Mwezi.

Mnamo Aprili, Shirika la anga za mbali lilitoa kandarasi ya $ 2.9bn kwa Elon Musk, na kukataa zabuni kutoka kwa kampuni ya Bezos ya Blue Origin.

Kandarasi hiyo ni kwa ajili ya kujenga mfumo wa kutua kwa chombo kitakacho wabeba wanaanga kwenda kwenye mwezi kuanzia mapema mwaka 2024.

Nasa ingeweza tu kutoa kandarasi hiyo kwa kampuni moja, na wala sio mbili kama ilivyotarajiwa kwasababu ya upungufu wa fedha.

Shirika hilo la Nasa lilikuwa limepokea $ 850m tu kati ya $ 3.3bn ilizokuwa imeomba kutoka kwa Bunge kujenga mfumo was kutua kwenye mwezi.

Katika barua kwa msimamizi wa Nasa, Bill Nelson, iliyotolewa Jumatatu, Bwana Bezos aliandika: "Blue Origin itapunguza bajeti yake ya fedha kwa kuondoa malipo yote ya kipindi cha sasa na miaka miwili ijayo ya fedha ya serikali hadi $ 2bn kuweza kuboresha mpango huo kwa sasa.

"Ofa hii sio ya kuahirishwa, lakini ni msamaha wa moja kwa moja na wa kudumu wa malipo hayo".

jb


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...