Search This Blog

Tuesday, July 27, 2021

Serikali ya Tunisia yaweka amri ya kutotoka nje usiku

Rais wa Tunisia Kais Saied ameweka amri ya kutotoka nje majira ya usiku kwa kipindi cha mwezi ujao, siku moja baada ya kulisimamisha bunge.

Pia amewafuta kazi mawaziri zaidi wa serikali baada ya kufutwa kazi kwa Waziri Mkuu Hichem Mechichi Jumapili.

Rais amekanusha madai ya chama kikubwa cha kisiasa, Ennahdha, kwamba alifanya mapinduzi. Alisisitiza alikuwa amefuata katiba.

Bwana Saied aliwahimiza watu wasiingie barabarani kuandamana, akisema hatari kubwa ni ya "mlipuko wa ndani".

UN imeelezea wasiwasi wake juu ya hali ilivyo nchini humo ikisema "mizozo yote na kutokubaliana inapaswa kutatuliwa kupitia mazungumzo", msemaji wa Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres alisema.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amemtaka rais wa Tunisia "kuzingatia kanuni za demokrasia na haki za binadamu" na "kudumisha mazungumzo ya wazi na wahusika wote wa kisiasa", msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani Ned Price alisema katika taarifa.

Kwa miezi kashaa sasa kumekuwa na mivutano ya kisiasa nchini Tunisia, hasa kuhusu namna ambavyo serikali inavyoshughulikia janga la virusi vya corona na mgogoro wa kiuchumi.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...