Search This Blog

Tuesday, July 27, 2021

Aliyekuwa rais wa Ivory Coast Gbagbo kukutana na rais Ouattara

 Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara Jumanne atakutana na mtangulizi wake Laurent Gbagbo.

Huu utakuwa mkutano wao wa kwanza tangu ghasia za baada ya uchaguzi mnamo 2010 ambazo zilisababisha vifo vya maelfu ya watu na mamilioni wakikimbia makazi yao.

Mkutano huo utafanyika katika ikulu ya rais.

Bwana Gbagbo hivi karibuni alirudi nchini humo baada ya kuachiliwa bila hatia na mahakama yakimataifa ya Jinai ICC

Viongozi wote wamekuwa wakihimiza kudumishwa kwa amani na maridhiano.

Msemaji wa Bw Gbagbo amenukuliwa akisema kuwa viongozi hao wamekuwa wakiongea kwa simu kwa wiki kadhaa kabla ya mazungumzo ya Jumanne.

Bwana Gbagbo hivi karibuni alitangaza kwamba yeye na rais mwingine wa zamani Henri Konan Bédié walikuwa wakiungana kumpinga Rais Ouattara.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...