Search This Blog

Thursday, July 15, 2021

‘Mshukiwa akiri jinsi alivyowaua watoto 13 na alivyowafyonza damu waathiriwa'


Polisi nchini Kenya wamemkamata mshukiwa wa mauaji mwenye umri wa miaka 20 anayedai kwamba amewaua watoto kumi na tatu katika msururu wa visa vya utekaji nyara na mauaji .

Mshukiwa huyo aliyetambuliwa kama Masten Milimu Wanjala aliwaelekeza maafisa wa polisi katika sehemu mbalimbali alikoitupa miili ya waathiriwa wake baada ya kuwaua katika tukio ambalo limewashangaza wengi.

Idara ya jinai kupitia twitter imechapisha taarifa ya simulizi ya mshukiwa huyo na jinsi alivyokuwa akitekeleza mauaji ya kikatili ya watoto ka kuwahadaa wanapokuwa wakicheza.

Polisi wamesema mbinu zake za kutekeleza mauaji ni za kuogofya na amekiri kwamba amekuwa akitumia kemikali inayofanana na unga kwa wathiriwa wake kabla ya kuwaua kwa kuwanyonga au kuwafyonza damu kupitia mishipa .

Miili ya waathiriwa wake wawili ilipatikana katika eneo la Kabete,viungani mwa jiji la Nairobi kisha mwili mwingine ulipatikana jana karibu na eneo hilo hilo pembezoni mwa mto.

Polisi wanasema mshukiwa alianza kutekeleza mauaji ya watoto akiwa na umri wa miaka 16,alipomuua msichana mwenye umri wa miaka 12 aliyetoweka katika Kaunti ya Machakos ,kilomita takriban 54 magharibi mwa mji mkuu Nairobi .

Polisi wamesema wanaendelea kumhoji mshukiwa ili kutambua sehemu nyingine alikoweka miili ya waathiriwa wake . Wachunguzi wamesema mwanaume huyo aliwaambia kwamba alikuwa akiwafuata watoto hao baada ya kucheza nao kwa muda .

Alikamatwa katika mtaa wa Kitengela mjini Nairobi baada ya uchunguzi kubaini kwamba alikuwa katika sehemu moja ambako watoto wawili walitoweka .

Visa vya kutekwa nyara kwa watoto vimeongezeka mjini Nairobi na polisi wamefanikiwa kuwaokoa watoto kadhaa lakini wengi wamekuwa wakipatikana wameuawa . Polisi maajuzi wameunda kikosi maalum cha kuchunguza na kusuluhisha kei za utekaji nyara jambo ambalo wanasema linatishia usalama wa taifa .



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...