Search This Blog

Thursday, July 15, 2021

Kigali yawekewa tena marufuku ya kutotoka nje


Serikali ya Rwanda imetangaza marufuku ya kutoka nje ya muda wa siku 10 katika mji mkuu wa Kigali na wilaya nane baada ya ripoti za vifo na wagonjwa wa corona kuongezeka.

Watu wametakiwa kutotoka nje ya nyumba zao kuanzia Jumamosi tarehe 17 mpaka tarehe 26 Julai, ili kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

Biashara, shughuli za umma na usafiri, shule, michezo na burudani vyote vimefungwa na mazishi yanatakiwa kuhudhuriwa na watu 15 tu.

Watu wanaweza kutoka nje ya nyumba zao kwa ajili ya huduma muhimu pekee au wafanyakazi muhimu.

Wiki nne zilizopita, taifa hilo limerekodi watu elfu moja waliopata maambukizi ya corona kwa siku na siku saba zilizopita hali ilikuwa mbaya zaidi.

Maofisa wa afya wamesema kusambaa kwa wimbi la tatu la kirusi kipya cha Delta ndio kinafanya taifa hilo kuwa na hali mbaya zaidi.

Rwanda imerekodi visa zaidi ya 50,000 vya covid , na zaidi ya waathirika 600 na huku zaidi ya watu mia nne wamepata chanjo.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...