Search This Blog

Thursday, July 15, 2021

DC Kayanda afanya ziara katika tarafa ya Eyasi na kujionea ukarabati wa zahanati ya Jobaj


 Mkuu wa wilaya ya karatu Mh. Abbas Kayanda akiwa na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama amefanya ziara katika tarafa ya Eyasi na kutembelea na kujionea ukarabati wa zahanati ya Jobaj na utekelezwaji wa mradi ya maji inayotekelezwa  na mamlaka ya usambazaji maji vijijini Ruwasa. 

katika ziara hiyo Mh. Kayanda ameshiriki kuchimba mtaro kupeleka maji katika kitongoji cha Antsaa katika kijij cha Mang’ola  barazani. amepongeza jitihada za wananchi katika kujitolea nguvu kazi  katika kusaidia utekelezaji wa mradi wa maji. Amesema serikali itasaidia kuchimba  eneo lenye mawe kiasi cha km 2 ili kusaidia ulazaji wa bomba kuu la kusambaza maji kwenye matanki mawili.

Mh. Kayanda ametembelea mradi wa maji wa  Mbuga nyekundu kujionea maendeleo ya mradi huo unaofanya kazi kwa nguvu za jua (Solar power). Ametoa rai kwa viongozi wa jumuiya ya maji na viongozi wa serikali ya kijiji kulinda kutunza miundo mbinu ya mradi huo wa maji ili isije ikahujumiwa. Katika hatua nyingine Mh. Kayanda amejionea rola za mabomba ambazo zinatarajiwa kutumika kusambazai maji mara baada ya ujenzi wa tank la kusambazia maji.

Katika hatua nyingine Mh. Kayanda ametembelea na kujionea ukarabati uwa zahanati ya Jobaj iliyopewa fedha kiasi cha million 50 na serikali. Mh. Kayanda ameonesha kutoridhishwa na matumizi ya fedha katika ukarabati wa zahanati Jobaj hivyo kuelekeza takukuru kufanya uchunguzi ili kujiridhisha kama ukarabati wa zahanati hiyo unaendana na thamani ya fedha iliyotolewa. Wakati huo huo Mh. Kayanda amemuagiza mganga mkuu wa wilaya kufanya ukaguzi wa dawa kila baada ya miezi mitatu kwa vituo vyote vya utoleaji wa huduma za afya katika wilaya ya Karatu, ili kujiridhisha na matumizi ya utoaji wa dawa. Amesema hayo baada ya kubaini utunzaji duni wa kumbukumbu wa dawa zinasosambazwa  na Msd nakutolewa kwa wagonjwa katika vituo vya afya.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...