Mjane wa rais aliyeuawa wa Haiti Jovenel Moise ameshutumu mauaji ya mumewe kwa kusema maadui walilenga kusitisha mabadiliko ya demokrasia.
Akizungumza katika video iliyochapishwa katika mtandao wa Twitter, Martine Moise ambaye pia alijeruhiwa wakati wa shambulizi hilo amesema mumewe alilengwa kwa ajili ya siasa.
Hayati Moise wakati wa machafuko aliwakasirisha wanasiasa wapinzani kwa kujaribu kuleta mabadiliko katika mikataba ya serikali na siasa na alipendekeza kura ya maoni ya kubadilisha katiba ya Haiti.
Huku hayo yakiarifiwa viongozi wa magenge nyenye nguvu nchini humo wamesema watafanya maandamano kupinga mauaji hayo na kutishia machafuko zaidi.
Akizumgumza kupitia video kiongozi wa shirikisho la G9 lenye magenge 9, Jimmy Cherizier, askari wa zamani aliyejulikana kama Barbeque alitukana polisi na wanasiasa wa upinzani na kuwashutumu kwa kushirikiana na mabepari kumtoa kafara Moise.

No comments:
Post a Comment